Hitmaker wa Roho Yangu, Richie Mavoko amesema anajua kile ambacho
Diamond Platnumz anawashikia watu, na yeye anajua kipi cha kufanya, ndio
maana anaonekana kuwa tishio kwake.
Akiongea na Bongo5, Richie Mavoko amesema alianza kumsikia Diamond
tangu akiwa shule na kwamba hakatai kuwa kuna vitu alijifunza kutoka
kwake.
“Mimi Diamond anatoka, mimi nipo shule, kwahiyo kuna vitu vingi
nimeviona, labda yeye amepitaje, amekosea nini na mimi nifanyeje ndio
maana mara nyingi mimi naonekana noma kwasababu mimi nishajua wao
wanataka nini. Yaani mimi nishajua anapowashkia watu halafu mimi nshajua
natakiwa nifanye nini,”alisema.
Mavoko aliendelea kudai kuwa muziki wake na wa Diamond haufanani hata
kidogo. “Mimi na huyo jamaa hatufanani kabisa yaani, sisi ni watu
wawili tofauti. Wote tunaimba Bongo Flava, Wote tunafanya kitu kimoja
lakini makoo tofauti sababu koo la Diamond sio koo langu mimi tuko
tofauti kabisa.”
Muimbaji huyo aliongeza kuwa hana urafiki wowote na Diamond licha ya kwamba wakikutana husalimiana.
“Mimi nachoamini sina ushkaji naye, sio lazima kuwa na ushkaji naye
lakini ni mtu ambaye ananijua, namjua ‘hi mambo, vipi poa, salama’
hatuna matatizo yaani.”
Source: Bongo5
0 comments