,

UNAMJUA JACKLINE WOLPER VIZURI??? HISTORIA YAKE IKO HAPA

6:47 AM



Anaitwa Jacqueline Wolper. Ni mmoja kati ya warembo wenye umaarufu wa aina yake nchini na kwenye “industry” ya bongo movies. Jack ni mwanadada mwenye mvuto unaokubalika na wengi na ameweza kujipatia umaarufu mkubwa sana kupitia Filamu  mbalimbali alizoshirikishwa na mpya alizoanza kuzifanya chini ya kampuni yake mwenyewe. Licha ya kuwa mwigizaji mwenye uwezo wa kipekee, Jack pia ni mwongozaji mzuri wa Filamu na mwandikaji “script” mwenye viwango vya kimataifa.


Jacqueline Wolper alizaliwa tarehe sita (6), mwezi wa kumi na mbili (12) wa mkoani Moshi –Kilimanjaro na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mawenzi huko huko moshi na baadaye elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Magreth ekenywa iliyopo jijini Arusha na baadae nchini Kenya.

Baada ya kumaliza elimu yake hiyo ya sekondari Jackline aliamua kujiendeleza kwa kusomea mambo ya “sales and marketing” na baade alianza kujihusisha na biashara za promotion na baadae allingia kwenye biashara za saluni maeneo ya tandale jijini Dar es Salaam, kabla ya kujiingiza kwenye sanaa ya uigizaji.

Jack aliingia kwenye sanaa kupitia kwa mwanadada Lucy komba ambaye pia ni mwigizaji mwenzake ndani ya tasnia ya bongo movies nchini. Yeye mwenyewe anasema kuwa Lucy ndiye aliyemfuata na kumshawishi ajiunge naye kwenye maigizo kwani anaona anaweza na atafanya vizuri kama ataamua kujiingiza kwenye sanaa. Kufahamiana kwa wawili hawa kulitokana na wao kuwa majirani na kwa Lucy kuwa mteja wa mara kwa mara katika “saloon” ya mwanadada Jack. Hii ilikuwa ni mwaka 2009.
Baada ya kushauriwa kwa muda mrefu ndipo Jack alipoamua kujiingiza kwenye sanaa na kwa mara ya kwanza alionekana kwenye Filamu ya “Ama Zangu Ama zao” aliyoifanya na mwanadada Lucy Komba.
Baada ya hapo alianza kupata mialiko toka kwa watu mbalimbali ili aweze kuigiza kwenye Filamu zao ikiwemo Wiliam Mtitu pamoja na Marehemu Steven Kanumba na aliweza kufanya Filamu mbalimbali zilizomjengea jina ndani na nje ya nchi  zikiwemo Red Valentine na Pusi na Paku.
Akiwa nyumbani jackline wolper katika muda wa mapumziko, hupendelea kujifunza kupiga gitaa, ushauri alioupata toka kwa marehemu steven Kanumba na pia hupenda kupumzika na kufanya usafi wa nyumbani kwakwe. Mida ya jioni huependelea kwenda kuogelea na kwenda kutazama movie kwenye sehemu za cinema.

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....