SIRI imefichuka! Mume (bado talaka) wa mwanamitindo maarufu Bongo
ambaye kwa sasa yuko korokoroni Macau nchini China kwa msala wa
kukamatwa na unga, Jacqueline Fitzpatrick Cliff,
Abdulatif Fundikira
‘Tifu’ anadaiwa kumnasa kimalavu Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
Mume wa Jack Patrick akiwa na Salha Israel.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Tifu, wawili hao hivi sasa wako
kwenye ‘mahaba niue’ na wote wawili wako tayari kufunga ndoa kwani
wazazi wa pande zote wamebariki ndoa hiyo.
“Salha sasa hivi humwambii kitu kwa Tifu na kila mmoja yuko tayari
kwa ajili ya kufunga ndoa na mwenzake. Lakini sisi kama marafiki wa
karibu tunaona ni jambo la heri,” kilisema chanzo hicho
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa huko nyuma Tifu alikuwa hana
imani kabisa na wanawake tena baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na
aliyekuwa mke wake, Jack Patric, kiasi ambacho alisema hawezi kuoa tena.
Rafiki huyo alisema kuwa baada ya Tifu kukutana na Salha aliona ndiye
anaweza kuwa mke bora (wife material) na kuamini kuwa hawezi kumtenda
kama alivyofanyiwa huko nyuma.
Salha Israel katika pozi.
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Tiff ili kupata
ukweli wa madai hayo ambapo bila kukanusha alisema kuwa ni mapema
kulizungumzia hilo kama yatakuwa tayari ataweka wazi.
“Kwa kweli hilo jambo ni mapema mno kulizungumza kwa hivi sasa lakini
mambo yakikuwa tayari nitaweka wazi kila kitu,” alisema Tifu.
Kwa upande wake Salha Israel alipopatikana kwa njia ya simu na
kuelezwa kuwa Ijumaa Wikienda lina hadi picha zao za kimahaba
alifunguka: “Ni kweli namfahamu, ni mtu wa karibu lakini ni sawa na kaka
yangu pia. Hayo mengine labda mumuulize yeye.”USIACHE KUSOMA HAPA, KARIBU TENA NA TENA. ASANTENI
0 comments