,

SOMA SIMULIZI HII YA WEMA SEPETU AKIELEZEA JINSI KIGOGO 'CK' ALIVYOMFILISI

1:23 AM


Wema Sepetu.
Wema hakuwahi kurudi kwenye ofisi yake baada ya kigogo wa ikulu kuchukua vitu vyote
WIKI iliyopita tuliishia pale Wema alipoweka wazi kuhusu kilichotokea baada ya kupanda kwenye jukwaa Leaders Club jijini Dar ambapo mpenzi wake Diamond alikuwa akiangusha shoo ya nguvu.
Alisema mama yake alikasirika sana na pia baadhi ya ndugu walimpigia simu na kumshangaa kwa alichokifanya kwa sababu walikuwa wanamjua kigogo wa Ikulu ‘CK’ ndiye mpenzi wa Wema.
Wiki hii anaendelea…
Mwandishi: Sasa baada ya kusikia CK kachukua vitu vyote ofisini kwako Mwananyamala, ulichukua hatua gani?
Wema: Mmmh! Unafikiri ningefanya nini sasa? Nilibaki nikisubiria tu nini kitaendelea.
Mwandishi: Alivyochukua vitu vyote pale ofisini, wewe hukuweza kwenda tena pale?
Wema:  Ningeendaje? Maana yeye ndiyo kila kitu, hata mkataba pale aliandikishiana na mwenye nyumba, nisingeweza kwenda tena.
Mwandishi: Baada ya vitu vyote kuchukuliwa ambavyo ndiyo vilikuwa moja ya vitega uchumi vyako, maisha yanaendaje?
Wema: Maisha yanaendelea kwa sababu tayari niliamua kuweka hadharani mapenzi yangu na Diamond, hivyo yeye aliniambia niondoe hofu ataniingizia vitu vingine.
Mwandishi: Sasa ameshavinunua vitu hivyo alivyokuahidi?
Wema: Bado, lakini nafikiri hivi karibuni mambo yatakuwa safi.
Mwandishi: Naamini kabisa hapo unapokaa alipagharamia CK, sasa huogopi akija Diamond sehemu ambayo imelipiwa na mtu mwingine?
Wema: Lakini hata kama alilipia yeye si ilikuwa ni kwa ajili yangu, sidhani kama kuna tatizo lolote katika hilo maana akifanya hivyo nitashangaa sana.
Mwandishi: Baada ya wewe na Diamond kurudisha mapenzi yenu ni nini matarajio yenu maana yeye ndiye aliyesababisha kila kitu kuchukuliwa?
Wema: Ni kwambie kitu, kila siku naamini kwa Mwenyezi Mungu  kama bahati yako ipo ipo tu, hivyo kama vile vitu vilichukuliwa vitarudi kwa njia nyingine maana mimi niliangalia moyo wangu unapopenda. Matarajio yetu ni kuzeekea ndani ya uhusiano na si vinginevyo.
Mwandishi: Sasa kitendo kile hukuona kama kiliikwaza familia yako, hasa mama yako mzazi?
Wema:  Naelewa sana kuwa nilimuumiza mama yangu lakini mwisho wa siku lazima nao waelewe kuwa hata ndege hutua kwenye mti wa aupendao.
Mwandishi: Mna mpango wa kufunga ndoa hivi karibuni?
Wema: Inshalaah…ndiyo dua yetu ya kila siku  Mungu akipenda tutafanya hivyo.
CREDIT - GPL

#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....