featured,
wasanii
NDOA YA DIAMOND NA WEMA NDIO HIYOOO, KUFANYIKA UWANJA WATAIFA. DIAMOND AITANGAZA
8:27 PM
KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za mauzo
nchini ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi kipya
Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema
Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na
Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza
jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo
yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata
ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani
wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili
kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije
tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije
tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi
karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima
uvifiche, hata Mwenyezi Mungu
naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili
vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili
vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba
wake Wema Sepetu ambapo katika
mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.

Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati
mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna
tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi
kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
Jipange101.com
USIACHE KUSOMA HAPA, KARIBU TENA NA TENA. ASANTENI
0 comments