,

JK AMPA DIAMOND DEAL BAAB KUBWA, SOMA HAPA

2:17 AM

Hii ni bahati ya mtende kuota jangwani! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatajwa rais pekee anayetoa sapoti kwa wasanii ambapo safari hii amempa ulaji staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Ishu hiyo ilitokea mwanzoni mwa wiki baada ya kukutana jijini New York, Marekani huku kila mmoja akiwa na majukumu yake kwenye ardhi hiyo ya Rais Barrack Obama.
Ilisemekana kwamba JK kamkutanisha Diamond na meneja wa staa mkubwa wa muziki kutoka Marekani, Trey Songz.
Kuna madai kuwa lengo la kumkutanisha Diamond na jamaa huyo ni ili afanye kolabo na Trey Songz hivyo kumweka kimataifa zaidi kama ilivyo kwa P-Squire.
Ilisemekana kwamba kama kolabo hiyo itafanikiwa JK atakuwa ameshiriki kuiunganisha kwa asilimia zaidi ya 90.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. akiwa kwenye meza moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Stori hiyo iliambatana na picha zilizomuonesha JK akiwa karibu na meneja wa Trey Songz huku Diamond akiwasikiliza kwa umakini.
Ilisemekana JK alizungumza na wasanii hao kwa muda mrefu katika mazungumzo ambayo yalionekana mazito.
Habari zilieleza kuwa JK alifanya hivyo kwa sababu siku zote amekuwa akitoa sapoti kubwa kwa wasanii wake wa Tanzania.
Baada ya Diamond kukutana na JK kwenye kikao hicho kizito na meneja wa Trey Songz, Diamond aliandika kwenye kurasa zake za kijamii:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
“Wapi utapata rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa thamani ambao unatafutwa karibu na kila mtu duniani…akautumia kukusaidia kukukutanisha na kuku-connect na mdau mkubwa duniani katika tasnia uliyopo ili kuhakikisha tu unafikia malengo na ndoto ya kazi zako….
“Dah! Asante sana mh. rais, Mwenyezi Mungu akuzidishie na kukusimamia katika uongozi wako na siku zote za maisha yako.” 
-GPL
USIACHE KUSOMA HAPA, KARIBU TENA NA TENA. ASANTENI

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....