SAD!!! MTOTO AKUTWA AMETUPWA NA MAMA YAKE MARA TU BAADA YA KUZALIWA...SOMA HAPA
12:54 PM
Tukio hilo limetokea Aprili 16, mwaka
huu, ambapo wasamaria wema walifanikiwa kumuokoa mtoto huyo kisha
kumpeleka katika kituo kidogo cha Polisi kilichopo Bunju A, na baadaye
alihamishiwa katika kituo cha Polisi cha Wazo, ambapo pia ilikutwa barua
aliyoiandika mama wa mtoto huyo ikiwa karibu na mtoto huo.
Aidha aliandika barua yenye maelezo
mafupi yanayoelezea maisha yake, huku akielekeza lawama kwa mzazi
mwenzake ambaye hakumtaja jina kuwa amemtelekeza muda mrefu bila
kumpatia mahitaji muhimu kabla ya mtoto huyo kuzaliwa, hali iliyomlazimu
kuchukua uamuzi wa kumtelekeza mtoto huyo.
Aidha barua hiyo ambayo FikraPevu imeipata, inasema kuwa mama mzazi wa mtoto huyo alitaka kujiua kwa kunywa sumu, ingawa hakufanya hivyo.
“Sijamuacha kwa ubaya ninampenda
mwanangu sana ila kutokana na maisha yangu kuwa magumu, nimeamua
kumtelekeza hapa ili apate msaada kwa wasamaria wema, mzazi mwenzangu
kanikataa kuanzia kwenye mimba nimejaribu hata kutoa ila
imeshindikana” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Kwa mujibu wa barua hiyo inaeleza
kuwa mtoto huyo alizaliwa Machi 17, mwaka huu, katika eneo la Mistuni
kufukuzwa kila mahali, ambapo mtoto huyo hajawahi kupata chanjo ya aina
yeyote, ambayo inatakiwa kutolewa kwa mtoto mchanga ili aweze kupata
kinga ya kumkinga na maradhi mbalimbali.
Kati ya matukio hayo, 242 yalihusu ubakaji, vipigo vilikuwa 388, ndoa
za utotoni 42, kutelekezwa 96, mimba za utotoni 228, ambapo kwa upande
wa Tanzania Bara ukionyesha kuwa Wilaya ya Babati mkoani Manyara
inaongoza ikiwa na matukio 132.
Ripoti ya Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania, iliyotolewa na
serikali pamoja na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef)
mwaka 2011, ilidhihirisha kuwa msichana mmoja kati ya watatu na mvulana
mmoja kati ya saba nchini Tanzania hukumbwa na unyanyasaji wa kijinsia
kabla ya kufikisha umri wa miaka 18
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments