Staa
wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na mwenyekiti wa Klabu ya
Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ wameingia kwenye bifu zito
baada ya kutofautiana katika makubaliano ya kikazi.
Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mabishano wakati Steve Nyerere alipokuwa akiandaa .
filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo alipaswa kumshirikisha Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
“Batuli alipohoji kuhusu malipo, Steve
hakuweka wazi ndipo mambo yalipoharibika, kikanuka kisha Batuli akamvaa
kwa maneno kiongozi huyo na kudai hana sifa za kuwa kiongozi,” kilisema
chanzo chetu.
Ili kujiridhisha na madai hayo,
mwanahabari wetu alimwendea hewani Batuli ambapo alipatikana na kukiri
kuwa ametofautiana na Steve chanzo kikiwa ni filamu hiyo.
Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Aliponipigia simu nilimwambia sitaweza
kwenda kushuti kwa sababu hakuna makubaliano yoyote tuliyofanya ikiwemo
gharama, usafiri, mavazi na vinginevyo ndipo akamaindi na kuanza kulaumu
na kisha kukata simu,” alisema Batuli.
Ishu haikuishia hapo, taarifa zinadai
kuwa baada ya Steve kutofurahishwa na majibu ya Batuli, aliendelea
kumtumia meseji za kumlaumu ndipo Batuli alipochachamaa zaidi kwa kujibu
mashambulizi.
“Steve anapaswa akasomee utawala na
uongozi bora kwani hafai kuwa kiongozi, hana busara, kwa sababu kabla
sijagombana naye nilikuwa nikisikia maneno na majungu ila baada ya
ugomvi wangu na yeye nimegundua hafai,” alisema Batuli na kuongeza:
“Ananiambia mimi ni msanii mchanga
ilihali mimi kwenye kiwanda nipo kwa miaka kumi na nne na mwaka 2,000
wakati naanza yeye alikuwa anachekesha watu ili apate kula kwanza
nimemdharau kwa sababu amekuwa akinichonganisha na wasanii wa Bongo
Movie eti mimi nimewaambia wanajiuza.”
Baada ya Batuli kufunguka, gazeti hili lilimgeukia Steve Nyerere na kumsomea madai hayo ambapo alifunguka:
“Sipendwi na watu na sijui nini tatizo,
nikiwa kama dairekta nina uwezo wa kumchagua huyu nifanye naye kazi na
huyu kumuacha, yule (Batuli) kama analeta chuki basi zitakuja hivyo basi
ni nyingi tu,’’ alisema Nyerere na kuongeza:
“Kwa heshima niliyoitengeneza kwa miaka
32 alafu nije nigombane na mwanamke, kwanza nagombana naye nini?
Nashukuru nimepata ushauri, naendelea na kazi ya kutetea maslahi ya
Bongo Muvi kama ni filamu mimi nilishachezesha msanii mwengine.”
GPL
GPL
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments