WOLPER : SIWEZI KUOLEWA NA MTZ, NITAFANYA KILA NALOWEZA NIOLEWE NA MTU WA NJE
12:33 AM
STAA
wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa,
atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo
ambao hawathamini mastaa.
Akizungumza
na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu
moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao,
wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.
“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na
hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama
wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.
“Kule
bwana (hajataja nchi) mtu akimuoa staa, anampa kipaumbele. Anaweza hata
kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa na maisha ya mke wake
yanakuwa yenye amani lakini hapa kwetu tunadharaulika sana ndiyo maana
nimefikia uamuzi huu,” alisema Wolper na kuongeza:
“Unajua Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni
lakini wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa
sababu ya kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa
kabisa, mimi siwezi kuolewa na Mbongo.”
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments