,

TAZAMA HIZI PICHA, MASTAA WA BONGO WAKIWA NA 'VISHTOBE VYAO'...BOFYA HAPA

10:41 PM


MWANAMUZIKI Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ aliwahi kusema ndoa si lazima lakini inaongeza heshima katika jamii. Kwa upande wa kiroho, kuoa au kuolewa ni agizo lililotolewa na Mwenyezi Mungu katika maandiko matakatifu.

H.Baba na mkewe Flora.
Leo katika makala haya tunakuletea mastaa wa muziki na filamu Bongo wakiwa na ubavu wao, japokuwa ni wasanii lakini pia wana maisha ya ndoa.
Wapo mastaa wa kike ambao wameolewa na watu wa kawaida yaani ambao hawajihusishi kabisa na kazi ya sanaa. Pia wapo mastaa wa kiume ambao wameoa wanawake ambao siyo wasanii na pia wapo waliooana mastaa kwa mastaa.
H. BABA & FLORA MVUNGI
Hawa ni mastaa wa Bongo ambapo Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba’ ni msanii wa muziki wa kizazi kipya huku mkewe Flora Mvungi akiwa ni msanii wa filamu. Wawili hao walifunga ndoa mwaka jana.
Ndoa ya mastaa hao imekuwa ya furaha na amani huku mtoto waliyempata hivi karibuni akiwa ndiye kaongeza furaha ndani ya ndoa yao.
http://api.ning.com/files/cK9WvIaJNHHtVp7ENIvx4vm1YDgjnGQZbRqq3xjb93FwADses92RwiThOcBeyIXGq4JtmzvImNUhktHdVCOKxFx2x7fCwUeB/KajalacropHarusi.jpg
KAJALA & FARAJA
Kajala ni msanii wa filamu Bongo. Alifunga ndoa na Faraja Chambo miaka kadhaa iliyopita baada ya kutengana na Prodyuza P-Funk.
Ndoa ya Kajala na Faraja ilikuwa ya furaha lakini iliingia doa baada ya mumewe ambaye alikuwa akifanya kazi benki kukumbwa na kesi ya kuujumu uchumi ambapo mpaka sasa anatumikia kifungo huku Kajala akiachiwa huru baada ya kulipiwa faini ya Sh, milioni 13 na msanii mwenzake, Wema Isaac Sepetu.
JB & MKEWE
Jacob Steven ‘JB’ amedumu na mkewe kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 na imekuwa ya furaha na amani kwani haijawahi kuripotiwa kuwa na migogoro kama za baadhi ya wasanii ambazo mwisho wake huishia kusambaratika.
TEMBA & MKEWE
Amani Temba ‘Mh.Temba’ ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo. Alifunga ndoa miaka kadhaa iliyopita. Temba na mkewe (jina halikupatikana mara moja) wanaishi kwa furaha na ndoa yao haikuwahi kuripotiwa na misukosuko yoyote huku ikijibu kwa mtoto mmoja.
MARLAW & BESTA
Lawrence Marima ‘Marlaw’ na Besta Gasper ni mastaa wa muziki wa kizazi kipya Bongo ambao walifunga ndoa miaka kadhaa iliyopita huko jijini Arusha. Ndoa ya wawili hao ambao kwa sasa wana mtoto mmoja ni ya furaha tele.
JACK PENTZEL & GADNA
Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ ni msanii wa filamu Bongo. Miaka miwili iliyopita alifunga ndoa na jamaa aliyetajwa kwa jina la Gadna Dibibi. Mwanzoni ndoa yao ilitikisika kutokana na skendo kwamba Gadna alikuwa mume wa rafiki yake Jack lakini kwa sasa hali ni shwari na maisha yao yanaendelea vizuri.
MTITU & MKEWE
Mtitu ni msanii wa filamu ambaye alifunga ndoa mwaka mmoja uliopita na mkewe ambaye anafanya kazi tofauti na sanaa. Wawili hao wanapendana na wanaheshimiana. Hivi karibuni furaha yao iliongezeka ndani ya nyumba yao baada ya kupata mtoto.
Suzan Lewis ‘Natasha’ katika pozi na mumewe Alex Humba Lumila siku ya ndoa yao.
NATASHA & MUMEWE
Mwanamama Suzan Lewis ‘Natasha’ ambaye ni msanii wa filamu Bongo alivunja ukimya hivi karibuni na kufunga ndoa ambayo ilikuwa gumzo midomoni mwa watu kutokana na kuolewa akiwa na umri mkubwa (miaka 46). Natasha aliwahi kukiri kwamba anayafurahia maisha ya ndoa kwani ni matamu kuliko yale ya kuwa singo.
RICHIE & MKEWE
Japokuwa baadhi ya wanawake huogopa kuolewa na wasanii, ndoa ya msanii Single Mtambalike ‘Richie’ na mkewe ambaye siyo msanii, imedumu kwa miaka mingi na wamejaliwa kupata watoto huku ndoa yao ikiwa na furaha na amani.
CREDITS :GPL
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....