,

SIASA ZETU: TUNDU LISSU AMSHUKIA LOWASA KWA MANENO MAZITO, SOMA HAPA

11:10 PM

KADA wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi, Edward Lowassa anadaiwa kutumia kigezo cha udini kutaka kuungwa mkono kwenye harakati za kukimbilia Ikulu jambo linalohatarisha amani ya nchi.

Aidha Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kuweka hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya ambayo aliwahi kulitangazia Taifa kuwa anayo vinginevyo itakuwa ni vigumu kuondoa mashaka kuwa si mshirika wao.  

Hayo yalisemwa juzi na Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Tundu Lissu na wakati akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Sombetini, Ally Bananga kwenye viwanja vya Ngusero.
Lissu alisema kuwa baada ya Lowassa kuona hana sifa za uongozi kutokana na kuwa si muadilifu wala safi kulingana na tuhuma za ufisadi zinazomwandama ameamua kukimbilia makanisani akiwashawishi viongozi wa dini wamuuunge mkono kwa kigezo cha kuwa ni Mkristo mwenzao.  

“Kuna makada wengine wa CCM nao wanazunguka huko misikitini wakisema hii ni zamu yetu sisi Waislam hivyo anashawishi wamchague kwa kigezo cha Uislam tu .Hawa watu wanasahau dini si kigezo wala sifa ya uongozi tuwakataeni, sijui wanalipeleka wapi hili Taifa zaidi wanatutafutia machafuko hawatufai wote hawa,” alisema Lissu.  

Akizungumzia muswada wa madiliko ya katiba, Lissu alisema kuwa katiba inasema kuwa nchi ni moja lakini kwa sasa kuna Maamiri Jeshi wawili ambao mmoja ni Mwenyekiti wa CCM, Kikwete na mwingine ni Makamu wake, Dk Mohamed Shein jambo alilosema kuwa ni hatari sana hasa ikitokea wakitofautiana na kupishana kauli ilihali wote wanamajeshi.
JUHUDI ZA KUMPATA LOWASSA KUZUNGUMZIA MADAI HAYA ZILIGONGA MWAMBA BAADA YA SIMU YAKE YA KIGANJANI KUPOKEWA NA MTU MWINGINE AKIDAI MBUNGE HUYO WA MONDULI YUKO KIKAONI AMBAPO ALITAKA APIGIWE BAADA YA SAA MOJA.
ALIPOPIGIWA TENA SIMU HIYO ILIITA BILA KUPOKELEWA

SOURCE : KANDILI YETU
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....