,

NIMEAMUA TU KUZIWEKA HIZI ILI NA NYIE MZIONE.....MAANA NDIO HABARI YA MJINI

11:41 PM

 


Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo.

Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.



Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji.

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akipiga gitaa kabla ya kumzawadia msanii wa muziki maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awilo.




Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.


Mmoja wasanii Mwimbaji na Mwigizaji wa filamu,ajulikanae kwa jina la kisani kama Dokii akiimba mbele ya umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM waliofika kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM,ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya


Kikundi cha TOT Plus kiongozwa na gwiji wa mipasho hapa nchini,Khadija Kopa wakiimba jukwaani.



JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.


Wasanii hao wa Filamu wakifurahia jambo jukwaani.


Nape na wanachama wengine wakiserebuka kwa raha zao.

Tunajua kuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na kila mtu ana haki ya kuchagua chama anachokipenda. Hawa wasanii wametimiza haki yao ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, lakini mie kama mtanzania pia nina haki ya kulijadili hili. Wasanii wetu siku hzi wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa kwa ajili ya manufaaa ya wanasiasa. Tuliona wasanii kama kina Marlow, walitumika sana na mwisho wa siku waliambulia maumivu mpaka kufukia hatua ya ksema hawataki tena siasa, Mie binafsi nawatakia kila la kheri katika njia waliyoichagua ila wawe makini tu na kile walichokifata..... #SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....