MWANAFUNZI mmoja (Jina limehifadhiwa umri wake ni 16) wa Darasa la Saba
katika Shule ya Msingi Mkombozi iliyopo katika mji mdogo Mbalizi Wilaya
ya Mbeya Mkoani hapa ameshindwa kuendelea na masomo tangu shule
zifunguliwe akiogopa kuzomewa na wenzie baada ya kuhisiwa kulawitiwa na
Mwalimu Mkuu wake.
Hatua ya mwanafunzi huyo kushindwa kufika shuleni kuungana na wenzie
kumetokana na madai ya kuzagaa kwa tuhuma za Mkuu wake wa shule
kumwingilia kimwili mwanafunzi huyo mwenye jinsia ya kiume wakati wa
masomo ya jioni(Twisheni).
Hii ndiyo ofisi ya mwalimu mkuu huyo ambayo ilikuwa inatumika kwa matendo machafu ya mwalimu huyo |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema atalifanyia kazi kutokana na kutokuwa Ofisini kwa wakati huo na kulitolea ufafanuzi unaotakiwa. |
Ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mbeya |
Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Mbeya, Dionice Boay alipoulizwa kuhusiana na tuhuma za Mwalimu wake alikiri kuzipata na kuongeza kuwa kutokana na Mwalimu huyo kufikishwa katika vyombo vya Sheria wao kama Ofisi hawana cha kufanya zaidi ya kusubiri Ripoti ya Polisi ambapo Mwalimu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma. |
Akizungumza
na waandishi wa habari Mwanafunzi huyo alisema Mwalimu wake huyo ambaye
alimtaja kwa jina la Lusekelo Thom, kuwa anatabia ya kumbakiza yeye
peke yake baada ya muda wa masomo ya jioni kuisha na ndipo huenda naye
ofisini na kuanza kumvua nguo.
Alisema
tatizo hilo limedumu kwa kipindi kirefu tangu Aprili Mwaka jana hadi
Disemba 27, mwaka jana baada ya bibi anayemlea kugundua (jina
limehifadhiwa kwa ajili ya upelelezi) katika mahojiano kutokana na
mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani kila siku tofauti na wengine.
Kwa
mujibu wa majirani wa Mwanafunzi huyo walisema kugundulika kwa maovu
anayofanyiwa na mwalimu wake kulitokana na upotevu wa fedha shilingi
20,000 na ndipo bibi huyo alipomuona mjukuu wake akiwa na mkebe mpya na
ndipo alipomuuliza kuhusu fedha zake ambapo Mwanafunzi huyo alikataa
kabisa.
Walisema
baada ya kubanwa zaidi alidai fedha za kununulia mkebe alipewa na
Mwalimu wake na amekuwa na kawaida ya kumpa fedha mwanafunzi huyo kila
siku ikiwa ni pamoja na kumwambia asilipe ada ya masomo ya jioni kwa
madai kuwa atakuwa anamlipia.
Alipobanwa
zaidi mwanafunzi huyo alidai kuwa baada ya kupewa fedha na mwalimu huyo
huenda naye ofisini na kufunga mlango kisha huvua nguo zake na
kumwamuru naye avue na kumlazimisha ashike nyeti za mwalimu wake huku
mwalimu naye akimshika shika na huo mchezo ulikuwa ukifanyika kila siku
na baada ya hapo mwalimu alikuwa akimrudisha mwanafunzi kwa bibi yake
majira ya saa mbili usiku.
Mashuhuda
wa tukio hilo na baadhi ya walinzi wa shule hiyo walikiri kuwepo kwa
tuhuma za udharirishaji wa Mwalimu huyo kwa Mwanafunzi kwa madai kuwa
kila siku Mwalimu huyo kujifungia ofisini na mwanafunzi ikiwa ni pamoja
na kuongozana naye kila mara.
Aidha
baadhi ya ndugu walisema baada ya kubaini hali hiyo walienda kutoa
taarifa katika kituo kidogo cha Polisi cha Mbalizi ambapo Jeshi la
Polisi lilimkamata Mwalimu huyo Januari 4, Mwaka huu na kufanya naye
mahojiano kisha kumpeleka mwanafunzi huyo Hospitalini kwa ajili ya
vipimo.
Hata
hivyo Mwalimu huyo alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alikataa
kuhusika huku majibu ya vipimo vya Hospitali vikionesha kutokuingiliwa
kimwili kwa mwanafunzi ingawa Maelezo ya mtoto alidai kuchezewa nyeti
zake kila siku na kwamba suala la kuingiliwa kimwili alikuwa
akilazimishwa lakini hakuweza kufanikiwa.
Mwalimu
huyo aliachiwa na jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha Mbalizi
alipokuwa ameshikiliwa kwa ajili ya mahojiano baada ya kuwekewa dhamana
na Mratibu wa Elimu kata ya Utengule Usongwe, Fredrick Silumbwe, na
kwamba upelelezi bado unaendelea ili kubaini kama kweli mwalimu huyo
anafanya vitendo hivyo huku kukiwa na taarifa kuwa Mwalimu huyo baada ya
tukio hilo alisafiri na kuelekea Kibaha Mkoani Pwani ambako yuko hadi
sasa.
Kwa
upande wake Mratibu Elimu kata alipoulizwa kuhusiana na tuhuma dhidi ya
mwalimu wake alisema hata yeye amekuwa anazisikia mitaani na kuhusu
kuweka dhamana alikiri kwa madai kuwa alipigiwa na baadhi ya walimu na
ndipo alipofanya hivyo kutokana na dhamana ni haki ya kila mtu.
Naye
Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Mbeya, Dionice Boay alipoulizwa
kuhusiana na tuhuma za Mwalimu wake alikiri kuzipata na kuongeza kuwa
kutokana na Mwalimu huyo kufikishwa katika vyombo vya Sheria wao kama
Ofisi hawana cha kufanya zaidi ya kusubiri Ripoti ya Polisi ambapo
Mwalimu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.
Alisema
kama ofisi hatua ya kwanza ni kumsimamisha kazi na kuteua Mwalimu
mwingine kukaimu Ukuu wa Shule ya Msingi Mkombozi wakati ofisi ikisubiri
taratibu za Kimahakama kutokana na tatizo hilo kuegemea kwenye makosa
ya jinai.
Aliongeza
kuwa Ofisi pia inatarajia kufanya ukaguzi katika shule hiyo ili kubaini
kama Mwalimu alikuwa na makosa mengine na kujua sababu ya Mwanafunzi
kutoenda shule hadi sasa licha ya wenzie kuendelea na masomo.
Hata
hivyo Kituo cha Haki za Binadamu kilionesha mshangao kutokana na
mtuhumiwa wa tukio hilo kuachiwa kwa dhamana ili hali upelelezi
haujakamilika na hakuna hatua zozote ambazo Jeshi la Polisi linaonesha
kulifanyia kazi ambapo mtuhumiwa alifikishwa Polisi Januari 4, Mwaka
huu.
Mwenyekiti
wa Kituo cha Haki za Binadamu Mkoa wa Mbeya, Said Madudu alisema Jeshi
la Polisi limechukulia suala hili kama ni siasa kwa kuchelewa kuchukua
hatua kwa wakati huku mtoto akiendelea kukosa haki yake ya msingi ya
masomo.
Aidha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipoulizwa kuhusiana na
tukio hilo alisema atalifanyia kazi kutokana na kutokuwa Ofisini kwa
wakati huo na kulitolea ufafanuzi unaotakiwa.
Hata
hivyo uchunguzi uliofanywa umebaini kuwepo kwa rushwa zinazopelekea
upelelezi wa kesi hiyo kuchelewa kutokana na kuwepo kwa taarifa za
Mtuhumiwa kutoa fedha shilingi Milioni Tatu ambazo bado haijulikani mgao
wake uliwagusa akina nani.
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments