matukio,
mpya
DUUH!! MREMBO ACHEZEA KIPIGO BAADA YA KUIBA SIMU NA KUIFICHA "MASJALA KUU", SEHEMU ZA SIRI...TAZAMA HAPA
3:39 AM
MREMBO
mmoja mkazi wa Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam (jina lake
halikupatikana) mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya
kuvamiwa na kudundwa baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mwanaume na
kuificha sehemu zake za siri.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, awali mrembo huyo alikuwa akila bata
na mwanaume aitwaye Hashim kwenye Baa ya Jassun Inn iliyopo maeneo ya
Mabibo huku mwanaume huyo akiwa ametandaza simu zake za kisasa juu ya
meza.
Imedaiwa
kuwa wakati wakiendelea kuponda raha, Hashim alikwenda msalani kwa
lengo la kujisaidia na kuacha simu zake mezani, aliporudi hakumkuta
mrembo aliyekuwa akiponda naye raha na simu yake moja haikuwepo.
“Jasho lilimtoka Hashim na kuwauliza watu waliokaa jirani alikoelekea mrembo huyo,” alisema shuhuda mmojawapo wa tukio hilo na kubainisha kwamba msamaria mwema mmoja alimweleza Hashim mwelekeo wa mrembo huyo.
Bila
kuchelewa Hashim aliwakusanya wapambe wake na kuanza kumtafuta mrembo
huyo na wakamnasa mita kama 150 kutoka Baa ya Jassun na kumuuliza kuhusu
simu iliyokuwa mezani lakini alileta ubishi.
“Walijitahidi
sana kumbembeleza ili aitoe simu kwa hiyari yake lakini alikataa, ndipo
Hashim na wapambe wakamwanzishia songombingo la nguvu na kufikia kumvua
nguo hadharani na simu ikakutwa kwenye nguo yake ya ndani,” shuhuda
wetu alisema.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, hadi kufikia kupatikana kwa simu
hiyo, mrembo huyo alikuwa hoi kutokana na vurugu aliyofanyiwa na wapambe
wa Hashim ambao walipoipata simu walimvisha nguo pamoja na wigi lake
lililokuwa limemvuka.Credit: Global publisher
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments