Ingawa
tendo la ndoa lisipofanywa kwa kuzingatia kanuni na taratibu, sambamba
na umakini, linaweza kusababisha maradhi, lakini kwa wanandoa, tendo
hilo linatajwa kuwa na manufaa mengi kiafya tofauti na faraja ya
kawaida iliyozoeleka kwa wengi.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu
cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Dk Yahya Kishashu anasema
inategemea tendo linafanywa na nani na mhusika yupo kwenye mazingira
gani.
“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa
msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na amekupa maandalizi
mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,”
anasema mtaalamu huyo.
Anaongeza kuwa ndiyo maana baadhi ya
watu wanatoka nje ya ndoa zao kwa sababu si mara zote tendo la ndoa
linawafurahisha wanandoa.
“Wakati mwingine tendo hilo laweza kuwa karaha kwao,” anasema
Mazoezi
Si hivyo tu, utafiti uliofanyika
Canada hivi karibuni umebainisha kuwa kufanya tendo la ndoa kwa kipindi
cha dakika 25 kwa wanamume kunachoma kalori 100 na kwa wanawake kalori
69.
Tendo hilo likifanyika kwa nusu saa,
linaweza kupunguza kalori za mwili kuliko kutembea kwenye mashine ya
mazoezi ya ‘treadmill’.
“Ni sawa na kucheza mpira wa tenisi
au kutembea ukipanda mlima kwa dakika 20 au kucheza gofu kwa kasi kwa
dakika 33 au zoezi la yoga kwa dakika 40,” sehemu ya utafiti hiyo
inasema.
Utafiti huo wa Canada ulishabihiana
na kampeni iliyofanywa na Taasisi ya Moyo ya Uingereza ambayo ilisema
kuwa dakika 30 za tendo la ndoa kwa siku ni muhimu kama mazoezi ya
kutembea kwa mashine.
Kwa undani zaidi utafiti huo ulichambua na kusema kuwa, tendo la ndoa, lina manufaa kwa moyo na mapafu.
Inaelezwa kuwa vichocheo
vinavyotoka baada ya tendo la ndoa vinasaidia kupunguza kiwango cha
msongo wa mawazo na kuongeza uzalishaji wa seli mpya za ubongo.
Kuhusu mazoezi, Dk Kishashu anasema
anakubaliana na utafiti huo na kusema kuwa ni kweli tendo hilo
linasaidia kupunguza kalori, lakini linapofanyika mara nyingi zaidi
linazeesha.
Hata hivyo, wanasayansi wanalipa
uzito mdogo tendo hilo katika muktadha wa ujenzi wa hisia na mwili na
kuwa halisisitizwi vya kutosha kama aina mojawapo ya mazoezi.
Tiba kwa moyo, mapafu na ubongo
Inaelezwa kuwa tendo la ndoa, linasaidia kuondoa msongo wa mawazo hivyo kupunguza hatari ya maradhi ya moyo.
Si hivyo tu, bali tendo hilo husaidia mapafu kufanya kazi yake vyema, kuingiza na kutoa hewa chafu.
Kitaalamu, upo mchakato uitwao
‘Neurogenesis’ ambao husaidia kulinda seli za ubongo zinazokufa kutokana
na uzee. Kuna eneo kwenye ubongo linaloitwa ‘hippocampus’ ambalo ni
eneo linalotengeneza kumbukumbu.
“Kazi kubwa inafanyika kwenye ubongo,
wakati wa tendo la ndoa, kiasi kikubwa cha viamsha raha huanzia kwenye
ubongo na kuleta taarifa kwenye maeneo mengine ya mwili.
Ndiyo maana watu wengi hupotea kiufahamu wakati wa kilele” anasema Dk Gosh, ambaye ni mtafiti.
Hata hivyo, wanaume ambao wanaendelea
na tendo la ndoa mara kwa mara hadi wanapofikisha miaka 50 na zaidi,
kwa maana ya kutoa mbegu za kiume mara kumi kwa mwezi, wapo katika
hatari ndogo ya kupata saratani ya tezi dume. Inaelezwa kuwa mbegu za
kiume hazitakiwi kukaa mwilini kwa muda mrefu.Zinatakiwa zitolewe mara
kwa mara ili kuzifanya seli mpya zizalishwe. Ni kama kusafisha mpira,
inasaidia kusitisha ujenzi wa seli za zamani ambazo zaweza kuwa chanzo
cha saratani.
Kwa wanawake, tendo la ndoa husaidia
kuundwa kwa misuli ya nyonga ambapo misuli hiyo ikiwa imara huondoa
hatari ya kushindwa kuzuia mkojo,(urine incotinence) jambo linaloathiri
mwanamke mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka zaidi ya 50.
“ Wakati wa tendo la ndoa, kwa
kawaida sakafu ya nyonga za mwanamke hubana na kuachia. Hii husababisha
misuli hiyo kuwa imara’ anasema mtafiti huyo.
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments