Linapokuja suala la mwenzi wa kufunga nae pingu za maisha, wengi hutaja sifa zinazotofautiana na sifa za boyfriend ama girlfriend wanaetaka kuwa naye.
“Kuishi na mwanaume mwenye meno 32, hukutoka naye familia moja, sio rahisi.” Aliwahi kusema mchungaji ambaye pia ni mbunge mwanamke aliyeteuliwa na Rais.
Kwa
kuzingatia hilo, mwimbaji wa kike ambaye pia ni muigizaji wa filamu za
Kiswahili, Shilole aka Shishi Bybee, alipiga story na tovuti ya Times Fm
katika kipengele cha Times Q & A, na kuelezea sifa za mwanaume
ambaye atafaa kuwa mumewe wa ndoa.
“Mimi
nampenda mwanaume mchapakazi, anayempenda Mungu. Mwanaume mweusi,
mwembamba lakini asiwe mwembamba sana…kawaida.” Shilole amefunguka.
Hata hivyo, Shilole ambaye ana watoto wawili amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuolewa.
“Watoto tayari ninao wawili, sina mpango wa kuolewa. Kuolewa ni maamuzi ila bado sijaamua, nikiamua ntaolewa tu.”
Shilole
ambaye mwaka jana alifanikiwa kupata show nchini Uingereza, ameachia
wimbo wake unaoitwa ‘Chuna Buzi’ na mashabiki wa muziki wake wanaonesha
kuulewa.
Credit:Times fm
0 comments