,

KAMA UNASIFA HIZI, BASI SHILOLE ANAKUTAKA UWE MME WAKE, SOMA HAPA

10:43 AM

 

Linapokuja suala la mwenzi wa kufunga nae pingu za maisha, wengi hutaja sifa zinazotofautiana na sifa za boyfriend ama girlfriend wanaetaka kuwa naye.

 “Kuishi na mwanaume mwenye meno 32, hukutoka naye familia moja, sio rahisi.” Aliwahi kusema mchungaji ambaye pia ni mbunge mwanamke aliyeteuliwa na Rais.

Kwa kuzingatia hilo, mwimbaji wa kike ambaye pia ni muigizaji wa filamu za Kiswahili, Shilole aka Shishi Bybee, alipiga story na tovuti ya Times Fm katika kipengele cha Times Q & A, na kuelezea sifa za mwanaume ambaye atafaa kuwa mumewe wa ndoa.
“Mimi nampenda mwanaume mchapakazi, anayempenda Mungu. Mwanaume mweusi, mwembamba lakini asiwe mwembamba sana…kawaida.” Shilole amefunguka.
Hata hivyo, Shilole ambaye ana watoto wawili amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuolewa.
“Watoto tayari ninao wawili, sina mpango wa kuolewa. Kuolewa ni maamuzi ila bado sijaamua, nikiamua ntaolewa tu.”
Shilole ambaye mwaka jana alifanikiwa kupata show nchini Uingereza, ameachia wimbo wake unaoitwa ‘Chuna Buzi’ na mashabiki wa muziki wake wanaonesha kuulewa.

Credit:Times fm
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....