, ,

INASEMEKANA DIAMOND KAHAMISHIA PENZI KWA HUYU MODEL, HEBU SOMA MWENYEWE

11:49 PM


Ama kweli wadada wa mjini wana mambo sana, wenyewe wanasema kua mjini shule kijijini kilimo. Sasa huku kuja kwa mitandao ya jamii kumeibua makubwa ambayo tulikua hatuyajui. Mwanzo Facebook ilikua ndo kila kitu kwa umbea wote wa town unaupata kule ila kwa sasa mambo yamebadilika kabisa, Insta ndo habari ya mjini. Kila kitu utakipata Insta hadi madalali lol.


Sasa habari tulizozipata kutoka huko huko insta ni kua baada ya Raisi wa wasafi bwana Diamond au Halima Kimwana anavyopenda kumwita Chibu Dangote kutemana na mwanadada DvjPenny na tetesi kusema kua Diamond wamerudiana na wema hili tulilolinasa laweza kuwashangaza wengi sana

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyrQjtmxjSup0xj5hjB9kVxH_1i1FGZ_34LROg32W_orDERYrQ5LbjIOZDP0GpeAF73yQRwT9mJKXa8mOZL-v617o_i4K67TaBV2saJRUvD-VyEFWyuo3LpoBlnqGCByWffTKZx6eqYwsZ/s1600/DIAMOND-WEMA.jpg
Habari zilizotafutwa na mdakuzi wa Bongoclan zinasema kua Bwana Diamond ana mtoto mpyaaa tena mkali ile mbaya. Katika pitapita yetu Insta tukakutana na post ya mtu mmoja hivi ambaye kila kukicha yeye ni kumtetea aliyekua X wa Diamond mwanadada Penny. Post hiyo iliandikwa "Uwiiiiii chaggabarbie aijasimama Bado hapo au nayo kibamia kwako ivi nimuulize diamondplatnum nae anayo kama hiyo nn eti wemasepetu vjpenny04 mana mnatoana macho kwa mtoto wa tandale sasaivi nasikia anapumzika kwa hamisa mobeto wanafata hii Kitu Kina dada tuambizane na dai nae anayo nini kama anayo ukitoka kwa hamisa nenda zamu chagga Basi uwiiiiii chaga una balaa ww Kitu na box ndomambo yako chagga be like keep calm its just a big di**"
 
Sifa kubwa ya mwenye hiyo akaunti ni kumtetea sana Penny na nahisi atakua ni mtu wake wa karibu kwani kuna vitu vingine anaandika ni vigumu kwa mtu ambaye si wa karibu na Penny kuvijua. Waswahili wanasema kua lisemwalo lipo na kama halipo basi laja, Je ni kweli Bwana Diamond anatoka na mtoto mzuri Hamisa????? Swali linabaki hapo???


Lakini kama utakua mfatiliaji mzuri wa mastory haya utakumbuka kua karibu mademu wote waliotembea na Diamond na baadae kujulikana ilianza kama tetesi hivi hivi, mfano mzuri ni Wema, Yule aliyekua demu wa Mr Blue, Penny, Jokate na wengine ambao ni ngumu kuwataja.
 
Kwa wale msiomjua Hamisa ni nani, ngoja niwape profile yake kwa ufupi tu. Hamisa ni Model. Umaarufu wake umeongezeka sana siku za hivi karibuni kwani kuna makampuni mengi yanamtafuta kufanya matangazo nae kutokana na uzuri alionao. Kwa wale mlibahatika kuliona Jarida la Pulse Kenya mwezi huu mwanadada Hamisa ndo alipamba ukurasa wa mbele.
 
Kama ni kweli Bwana Diamond kaamua kujituliza kwa Hamisa itakua poa coz mtoto kasimama kila idara, Unaweza tazama picha za mwanadada Hamisa zilizokusanywa na mdakuzi wa Bongoclan hapa chini.



CREDITS TO BONGOCLANTZ KWA MAUDAKU HAYAAA

#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....