,

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA HUKO MOSHI NA KUUA WATU KIBAO....SOMA HAPA

3:31 AM

breakingnewsTaarifa ambazo zimetufikia muda Mfupi uliopita zinasema Kuna ajali mbaya ya Barabarani imetokea Huko karibu na KIA Moshi ajali ambayo imehusisha Basi Dogo la Abiria aina ya Coaster na Lori la mizigo Aina ya Fuso ambapo yamegongana uso kwa uso na kusababisha vifo.
Coaster hiyo ilikuwa ikitoak Arusha kwenda Moshi ikiwa imesheheni Abiria wa kutosha inasemekana ilikuwa ikienda kwa mwendo kasi na Dereva kushindwa kuhimili kuyumba kwa gari hilo wakati ambapo akiwa katika mwendo kasi kitu ambacho kilifanya ashindwe kupishana na Lori hilo lililokuwa likitoka Moshi kwenda Arusha.
Shuhuda wa Ajali hiyo ambaye alikuwa akitoka Arusha kwenda Moshi ameongea na Haazu na kusema kuwa Kuna uwezekano kwa watu wachache sana kupona katika Ajali hiyo kwani hata sura za watu wengi hazijulikani huku Majeruhi wakiwa katika hali mbaya zaidi.
Kwa upande wa Dereva Shuhuda wetu amesema kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Dereva kafariki hapo hapo kwani upande wake ndio ulioathiriwa Zaidi.
Shuhuda wetu pia ilikuwa ahusike kwenye ajali hiyo kwani alilisimamisha gari hilo mara kadhaa ili asafiri nalo na Dereva hakusimama kitu kilichomlazimu kusubiri gari lingine na kusafiri nalo na Kufika Karibu na KIA ndipo alipokuta gari hiyo ikiwa imeisha.
MSIKILIZE HAPA CHINI SHUHUDA AKIONGEA NA HAAZU

#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....