,

MSANII HUYU WA BONGOMOVIE ALALAMIKA KUSUMBULIWA NA MAPEPO...

1:05 AM

Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
 NYOTA wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, amesema kila aingiapo kwenye kazi ya kurekodi filamu, anapatwa na tatizo la kupandisha maruhani (mashetani), jambo ambalo linamkosesha raha. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Batuli alisema kuwa hawezi kumhisi mtu yeyote vibaya juu ya tatizo hilo, lakini hali hiyo inamkosesha amani, kwani haelewi chanzo chake.
“Mimi kwa kweli sitaki kabisa kuweka imani tofauti ya kumhisi mtu vibaya, ila najiuliza kwanini nipandishe maruhani wakati wa kurekodi peke yake?” alisema Batuli.
Batuli aliongeza kuwa kinachomchosha zaidi, hata akienda hospitali haonekani kama ana tatizo lolote, hali ambayo inampa mawazo zaidi.
Aliongeza kuwa hana jinsi ya kufanya, kilichobaki ni kumuomba Mungu aweze kumsaidia ili aweze kuepukana na hali hiyo.
USIACHE KUSOMA HAPA, KARIBU TENA NA TENA. ASANTENI

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....