umezisoma hizi?
>> JE WAJUA MASTAR WENGI WA KIKE HUJITONGOZESHA KWA DIAMOND???? SOMA ALICHOKISEMA DADA WA DIAMOND HAPA. >> BABA MZAZI WA DIAMOND AZIDI KUMSHANGAA MWANAE KWA KUMTENGA, SOMA ALICHOKISEMA HAPA. >> MILIONI 13 ZAZUSHA TIMBWILI LA HATARII,WEMA NA KAJALA NGUMI NONDO NJE NJE WAPAMBE WAO WAINGILIA KATI. >> KUTANA NA MTU WA AJABU,CHAKULA CHAKE NI TOFALI PEKEE....tazama na soma zaid hapa >> Tazama picha jinsi kundi la MAFIKIZORO walivyo funika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar....jamaa hawa ni noma sanaaa >> AMA KWELI HUU MWAKA WAKE::COLLABO NYINGINE YA DIAMOND NA MWANAMUZIKI WA NIGERIA HII HAPA
JE WAJUA MASTAR WENGI WA KIKE HUJITONGOZESHA KWA DIAMOND???? SOMA ALICHOKISEMA DADA WA DIAMOND HAPA.
KUMBE! Aliyejipachika kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele, Halima Haruna ‘Kimwana’ amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha wenyewe kwa jamaa huyo.
Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya
kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.
Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka tuwatongozee kwa kaka yetu.
Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa
wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima.
Kama hiyo haitoshi, Halima Kimwana alianika kuwa, hajishughulishi na suala la uhusiano wa Diamond na atamheshimu kila msichana atakayetambulishwa KAMA WIFI HUKU AKITOLEA MFANO JINSI ANAVYOUHESHIMU UHUSIANO WA DIAMOND NA WEMA SEPETU KWA SASA.
-gpl
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments