,

HUYU NI KIONGOZI MKUBWA TU CCM LAKINA ALICHOKIANDIKA HAPA NI UPUUZI MTUPU, SOMA HAPA MWENYEWE

10:48 AM

 
@ LE MUTUZ LIVE STARIGHT TALK!!:- - Jana kuna Wabunge wawili wa CCM waliopiga kura za hapana kwenye hoja ya bunge ambayo msimamo wa chama Tawala ulikuwa ni NDIO, sasa seriously ni kwamba hawa wamekataa sera za chama wanachokisimamia kama Viongozi na wote wawili ni marafiki zangu sana wa karibu, lakini kwenye msimamo na sera hatuna urafiki ninaomba kuwaaambia wote wawili kwamba wakati muafaka wa kujitoa CCM na kwenda chama wanachokiamini ni sasa na hasa baada ya jana kwenda kinyume na sera ya chama chetu CCM.

- Hili wala halihitaji mjadala wala maelezo wameamua wenyewe kwa hiari yao kwamba hawataki kukubaliana na msimamo wa chama chetu sasa ni vyema wakaijunga na chama ambacho kitakidhi matakwa ya misimamo yao, sio mara ya kwanza sasa wote wawili wamekuwa wakitoa kauli tete sana kuhusiana na misimamo ya CCM, sasa Duniani kote ustaarabu ni unajitoa na kile chama huwezi kuishi kwenye ndoa ya kulia lia kila siku kuhusu ndoa ambayo hujalazimishwa na mtu, nawakumbusha tena wale Wabunge wawili kwamba CCM ni kubwa sana kuliko wao na haiwezi kutetereka kwa sababu ya Wabunge wawili tu no way, na kulinda heshima zao kwa jamii na hasa CCM wajiote sasa ndio watajijengea heshima kubwa na Taifa.

- Na kama hawajitoi wenyewe basi Kamati ya Maadili iaite na kuwaondoa mara moja waende kwenye chama ambacho kitakidhi misimamo yao sio CCM, haiiwezekani na haipo Dunia nzima, Senetor Liberman pamoja na kugombea Umakamu wa Rais wa USA alipoona chama chake kina msimamo asioutaka akajitoa na kuwa Independent, unaitwa uungwana sivyo unakuwa mnafiki na ndamakuwili, wote wawili nawaheshimu sana ni watu wangu wa karibu sana sana, lakini kwa hili naomba kuwaambia with my straight face kwamba wajitoe CCM, hatuwezi kuwaamini tena!!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!

Le Mutuz Safarini Chalinze!!


My take!! Katiba inayotengenezwa ni ya chama cha mapinduzi au Wananchi?? Kwa hili mheshimiwa umeteleza tena sana, kajifunze siasa upya. Usitake mawazo yako yafanane na ya wote, na hapo CCM ndio mnakosea. Katika kundi la watu, usitake kudominate na mawazo yako pekee, hii ndio Demokrasia na mtu anakuwa huru kuchagua kile anachoamini kuwa ni sahihi. Poleni sana CCM kwa mawazo yenu Mgando na ya kizamani. Na hongereni sana Ester Bulaya na Kange Lugola..nyie ndio watetezi wa wananchi na sio watetezi wa maslahi ya Chama. Keep it up

#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....