,

KUWENI MAKINI JAMANI, SIKU HIZI KUNA BIASHARA YA FUMANIZI..ANGALIA USINASE

10:13 PM

 
Nawatahadharisha,

kuna rafiki yangu baada ya kupigika na maisha toka mwaka juzi akapata wazo la kuanzisha biashara ya mafumanizi.

Ameajiri wadada 5 kinachofanyika anawatumia hao wadada kuandaa mafumanizi. Mkikubaliana na wadada yeye anakuja na watu wacamera na mabaunsa 2 kufumania pia watakutaka utoe pesa.

Ukitoa pesa anazotumia kulipa mishahara kwa kila mwezi kama faida yake hakosi million 5.

Huu ni mwaka wa pili sasa hivi amejenga na ana gari 2 za kutembelea pia ameoa.

Elimu yake ni kidato cha nne tu na wana ofisi kabisa. Makazi yao ni Dar lakin uwa wanasafiri adi mikoani.

Uwa wanatoza pesa kulingana na mtu alivyo. Wanatoza kuanzia laki 5 adi million 10.

Mbaya zaidi wanakupiga na picha hivo lazima utatoa pesa.

Mnaopenda wanawake wa barabaran kazi kwenu.

Source:Jamii Forums
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....