Unapenda
kufanyiwa massage na nyoka? Unaweza kukaza roho na usiogope kung’atwa?
Kama ndio basi nenda nchini Indonesia utaipata kwa raha zako.
Massage
hiyo inapatikana Bali Heritage Reflexology and Spa huko Jakarta,
Indonesia ambako wanaweza kukuondolea uchovu wako wa siku nzima kwa
massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.
Massage
hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya mwili wa mteja na mengine
huachiwa yeye nyoka afanya yake. Ili kupata huduma hii mteja hutakiwa
kulipa dola 47 ambazo ni zaidi ya shilingi 76,000 za Tanzania.
kutoka- Bongo5.com
0 comments