‘We Talking Money You Talking Nonsense’ huenda ikawa kauli nzuri kuelezea hiki walichokifanya P-Square kwa sasa.
Hakuna ubishi kuwa, kwa hiki
walichokifanya sasa, na kama macho yetu hayatudanganyi kwa hiki
yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama hii inayoonekana ni
dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.
Peter ameshare picha hizi nne ambazo
wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika ambapo kwenye picha moja
inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa amesimama kwenye sebule mpya
inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya, ameandika ‘Goldenworld #blessed.’
Kwenye picha nyingine, wanaoonekana
wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana
kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter ameandika: #2kings……
Work hard,play harder.’
Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa
peke yake kwenye meza ya chakula, kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya
kuvutia na ameandika: A king in my own world…. #Blessed.”
Hawa jamaa ni noma
CREDIT-BONGO5
0 comments