Baada ya kutoonekana katika pozi za kimahaba kwa muda mrefu, kwa mara ya kwanza, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu.
Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha zake za kimahaba tangu alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia’ ambayo yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo yalivyosomeka.
“Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake alizokuwa akichati na shoga yake kuhusiana na jamaa huyo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi alimtafuta sosi huyo na kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha kazi ya kuwasaka wahusika ikaanza.Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Gee ambaye kwa mujibu wa vyazo tofauti, ilidaiwa kuwa kwa sasa hayupo Bongo na hakuacha mawasiliano yoyote tangu alipoondoka.
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, mwanahabari wetu alimtwangia simu Wolper ambaye alikiri kuzifahamu picha hizo na kudai kuwa zilipigwa tangu mwaka juzi.....
Alipoulizwa kama jamaa huyo ndo baba watoto wake, Wolper alikana na kudai kuwa ni mshikaaji wake tu na kwamba picha hizo walizipiga wakiwa baa pindi alipokuwa akihamia Mwananyamala....
Kuhusu chatting yake akimsimulia rafiki yake kuwa jamaa huyo ni mume wa mtu, Wolper alikana pia na kudai hizo meseji ni za kutengeneza.....
Hii ni mara ya pili kwa Wolper kutuhumiwa kukwapua bwana wa rafiki yake. Hivi karibuni mshiriki wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid alilalamika kuwa Wolper kamchukulia bwana’ke aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa mastaa wengi wa kike hasa wa filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume kuwa sehemu ya utamaduni katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea heshima mbele ya jamii.
Source: Risasi Jumamosi/ Gpl
USIACHE KUSOMA HAPA, KARIBU TENA NA TENA. ASANTENI
Source: Risasi Jumamosi/ Gpl
0 comments