,

UTABIRI : WASANII WATAKUFA SANA MPAKA MWEZI APRIL MWAKANI

1:00 AM



Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mnajibu Afrika na kwingineko duniani, marehemu Shehe Yahya Hussein alisema:
  Nasisitiza tena, mwezi wa kinyota huanza Aprili na kuishia Aprili. Katika kipindi cha mwaka huu, kinyota inaonesha watakufa wasanii mfululizo hivyo ni vema wakachukua tahadhari na kukubaliana na hali halisi.
Alipoulizwa nini cha kufanya, Maalim Hassan aliendelea:
  Wasanii wanatakiwa kumuomba Mungu. Kama ni Muislam asikose kuswali msikitini, kama Mkristo asikose kuhudhuria kanisani na kama ni mpagani, basi atafute namna yake ya kumuomba mungu wake.
Mbali na Mungu, Maalim alikwenda mbele zaidi: 
  Pia kinyota wasanii wasivae nguo nyekundu kabisa. Wasipake rangi nyekundu midomoni (lipstick) na kwenye kucha zote. Kimsingi waachane na vitu vya rangi nyekundu.
Pia wasitoke kwenda kwenye starehe au shughuli za usiku hasa Jumanne na Jumamosi jioni kwani ni siku za vita kati sayari ya Venus na Mercury ambapo mkuu wake ni Israeli Mtoa Roho.
Alisema kuwa suala la vifo vya wasanii si kwa Tanzania tu kwani hivi karibuni tasnia ya filamu duniani imekuwa ikiondokewa na wasanii kibao kuanzia Hollywood (Marekani),
Nollywood (Nigeria), Bollywood (India) na hata nchini Kenya mwigizaji aliyeigiza kama Idd Amin kwenye simema ya Rise and Fall of Idd Amin amefariki dunia hivi karibuni hivyo ndiyo hali halisi kwa kipindi hiki hadi Aprili, mwakani.
Mbali na Tyson anga la bururudani Bongo  liliwapoteza wasanii wengine kama Shaila Haule ‘Recho’ Adam Philip Kuambiana na Amina Ngaluma.

MY TAKE : SIO MIMI BALI NI MANENO YA MTABIRI MAALIM HASSAN
USIACHE KUSOMA HAPA, KARIBU TENA NA TENA. ASANTENI

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....