Wakati vijana wengi mjini wakiangaika kupiga mzigo na kusubiri chao mwisho wa mwezi , ney wa mitego ameona isiwe tabu kujipa kazawadi kidogo cha kusherekea siku yake ya kuzaliwa. Unajua jamaa kanunua nini ? mshkaji kaangusha gari jipya aina ya Nissan Murano ikiwa ndio mara ya kwanza anafanya sherehe ya birthday.

Ney alinena haya kuhusiana na gari yake mpya “Nimejinunulia Gari Aina ya Murano Kama zaiwadi ya Birthday yangu , Limenigharimu Shilingi Mil 36 za Kitanzania , ni la Mwaka 2007 so bado ni Jipya Kabisa, One Love kwa mashabiki wangu”

0 comments