Mapenzi ni kitu Fulani tofauti sana
kwenye hii dunia na hata nje ya hii sayari. Mapenzi kwa kiasi kikubwa
sana yanasababisha hata mambo mengine kwenye hii
dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa mapenzi.
dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa mapenzi.
Ukiachilia mbali PESA, Mapenzi huwa
yana nafasi kubwa sana kwenye kitu chochote ndani yahii dunia
tunayoishi. Si masikini wala si tajiri, wote kwa pamoja wanahitaji
mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze kwenda sawa kwa upande
wao. Na ndio sababu hata mimi hapa ninaandika kuhusu mapenzi kwa sababu
yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa sasa.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na
kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama
kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata
matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na
kupendwa kwa dhati.
Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au
kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako
utaiona chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela
kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais.
Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa
kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae sana
wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza
kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine
hata kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na
hizi zifuatazo;-
1. UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo
kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa
dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa
sana miongoni mwa wanaopendana
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments