Alisema mwanamke huyo alitenda unyama
huo kwa mumewe majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Ipapa kata ya
Ipunga wilayani Mbozi. Mwanamke huyo alimuua mumewe kwa kumkata kisogoni
na kitu kinachosadikiwa kuwa ni panga kabla ya kumvunja shingo na mguu
wa kushoto. Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa
kimapenzi na kuwa kabla ya tukio wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa
kutuhumiana kuchepuka nje ya ndoa. yao. Mwanamke huyo atafikishwa
mahakamani baada ya taratibu kukamilishwa na kusisitiza kwa kuwataka
wanajamii kutumia njia ya mazungumzo kusuluhisha migogoro baina yao
badala ya kutumia mabavu.
USIACHE KUSOMA HAPA, KARIBU TENA NA TENA. ASANTENI
0 comments