HAYA
yanaweza kuwa ni mambo ya malovee! Kuna madai kwamba Mbongo Fleva
Nasibu Abdul ‘Diamond’ alishindwa kushiriki zoezi la kuuaga mwili wa
mwanamuziki mkongwe Tanzania, marehemu Muhidin Mwalimu Mohamed Gurumo
‘Maalim Gurumo’ kwa sababu alifungiwa asitoke ndani na mwandani wake
madam Wema Sepetu, Ijumaa linakudadavulia.
Imedaiwa kuwa, Wema
alimfanyia ‘umafia’ mpenzi wake huyo, Aprili 15, mwaka huu ambapo
ilikuwa ndiyo siku ya mwili wa marehemu huyo kuagwa nyumbani kwake
Mabibo jijini Dar na kwenda kuzikwa kijijini Masaki, Kisarawe, Pwani.
Itakumbukwa kuwa,
Diamond ndiye msanii aliyewahi kumpa zawadi ya gari marehemu Gurumo
kutokana na kuguswa na mchango wake katika tasnia ya muziki nchini.
Diamond akimsaidia mzee Gurumo kupanda stejini kabla ya kumkabidhi gari Agosti 29, 2013.
Kwa mujibu wa mashuhuda,
kitendo cha Diamond kutoonekana katika mazishi hayo ni kama
amejishushia heshima kubwa aliyojijengea pale alipomthamini marehemu
huyo kwa kumpa gari aina ya Toyota FunCargo.
“Tulitegemea tungemuona
msibani lakini kwa kutokuwepo kwake ni kama mchango wake wa kumpa gari
Gurumo hauna maana,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwepo msibani hapo.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.
Baada ya mapaparazi wetu
kufanya upekuzi yakinifu msibani hapo, walibaini kuwa, Diamond hakutia
‘maguu’ hivyo shughuli ya kumsaka ikaanza.
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.
Breki ya kwanza kwa mapaparazi wetu ilikuwa nyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.
Mapaparazi hawakuchoka,
wakahamishia ‘majeshi’ nyumbani kwa mwanandani wake Wema, Makumbusho,
Dar ambako mlinzi alibainisha kuwa, Diamond yupo na ‘bebi’ wake Wema.
Mapaparazi waliondoka na
kurudi tena saa 8:37 mchana ambapo pia waliambiwa wapendanao hao bado
wamejifungia ndani, wakaondoka hadi muda wa jioni baada ya shughuli za
mazishi, walirejea na kuambiwa Diamond alitoka muda si mrefu pasipo
kujulikana alikoelekea.
Waandishi wetu walimvutia waya Diamond lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.
Kusaka data zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda Kisarawe ambako mazishi yalifanyika.
Mzee Gurumo akionyesha ufunguo wa gari alilozawadiwa na Diamond.
“Tulikuwepo nyumbani kwa
marehemu. Nilikuwa mimi na Diamond tena tumefika muda huohuo ndiyo
mwili ukawa unapelekwa kwenye gari. Huwezi amini tulijumuika kuupandisha
mwili kwenye gari na sisi tukarudi nyumbani kuendelea na shughuli
zetu,” alisema Babu Tale.
Mapaparazi wetu baada ya
kutoshibishwa na maelezo hayo, juzi Jumatano walimtwangia simu Diamond
ambaye alizungumza kwa ‘kujikanyagakanyaga’.
“Mh! Nilikuwepo msibani
ila sikwenda kuzika tu maana nilikuwa na Babu Tale pale na tulikuwa
karibu kabisa na gari la Global Publishers, mara tu baada ya kumaliza
kuupandisha mwili wa marehemu kwenye gari tuliondoka na kurejea kwenye
majukumu yetu,” alisema Diamond.
Mapaparazi wa Global
walikuwa jirani na gari alilotaja Diamond lakini hawakumuona staa huyo
achilia mbali waombolezaji wengine ambao waliuliza kwa nini msanii huyo
hakufika kwenye msiba wa rafiki yake mkubwa!
Source:GPL
Source:GPL
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments