HIZI NDIZO TWEETS ZA MEYA WA ILALA ZILIZOZUA GUMZO NA KUWATIA HASIRA WATU...SOMA HAPA
10:43 AM
Japo mwanzoni alileta majibu ya dharau
baada ya kusoma 'tweets' hizo mbili za mwanzo hapo juu, lakini
akakumbana na hasira za wananchi wengi ambao hawakupendezwa na majibu
yake. Lakini kwa vile neno 'samahani' halipo kwenye kamusi za wengi wa
viongozi wetu, Mstahiki Meya 'aliingia mitini' kimyakimya...na
hajaonekana tena huko twitter hadi wakati ninaposti bandiko hili.
Swali la msingi: Hivi Katiba Mpya
tunayohangaika kuipata huko Dodoma itaweza kweli kutengeneza mazingira
yatakayowawezesha wananchi kuwashughulikia 'wahuni wa kisiasa'
(political thugs)? Jeuri kubwa inayowafanya watawala wetu kufanya
(including kusema) chochote ni kutochelea matokeo. Na japo Katiba tuliyo
nayo sasa ina sheria nzuri tu za kumpatia mwananchi kile anachostahili
(kwa maana ya haki zake), tatizo limebaki katika usimamizi wa sheria
hizo, na pengine kubwa zaidi, sheria hizo kubaki kama maandiko tu
yasiyoheshimiwa. Je Katiba Mpya (laiti ikipatikana) itaheshimiwa?
Finally, ninaamini Mstahiki Meya Silaa
nafsi itamsuta na atakatisha ziara yake huko Mwanza na kuungana na
wananchi katika harakati za kukabiliana na athari za mafuriko Dar (kwa
yeye ni Manisapaa ya Ilala). See, kwenda kumwona mgonjwa hakumaanishi
kutamfanya aopone bali kwaonyesha kuwa flani anajali. Kadhalika,
tunapokwenda kwenye misiba haimaanishi kuwa tutamfufua marehemu, lakini
ile tu kuwafariji wafiwa kunaonyesha kuwa tunajali. Nam ,Meya Slaa akiwa
Illa/Dar hatozuiwa athari za mafuriko (au kama alivyosema mwenyewe
"hawezi kzuwia mvua") lakini kibanadamu tu anapaswa kuwa na wahanga wa
mafuriko (japo yeye ana-pick and choose nani anastahili kuitwa mhanga)
By Kibo10
Source: JF
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments