Unaweza kuamini ukiambiwa kuwa, umaarufu hapa Bongo unakuja na rangi
yake ya kipekee, hata kwa watu wanaochipukia na kutamani kuwa maarufu
siku moja, wanaamini kuwa, ili kufanikiwa ni lazima kwanza uwe na rangi
nyeupe ya ngozi yako, huwezi kushangaa kwa hili sababu hata Lupita
Nyong’o pamoja na kufanikiwa kuwa mwanamke mwenye mvuto mwaka 2014, naye
alikuwa anaamini hilo alivyokuwa mdogo.
Hapa kwetu Bongo imekuwa kama ugonjwa vile wa kuambukizwa kati ya
watu maarufu na hata wale wanaochipukia, kujikuta wanatumia kila hali
kubadilisha ngozi yao, wapo wasanii wengi sana na watu maarufu, ambao
hutoweza amini uonapo jinsi walivyokuwa hapo nyuma na hivi sasa
wanavyoneka, kama ulikuwa hujui hili ni kwamba endapo mtu akibadilika
namna hii, ni vigumu kabisa kurudi hali yake ya zamani ya uhalisia.
Watu Wengi maarufu wamejikuta wakijutia kujibadili haswa pale miaka
inavyozidi kwenda, kutokana na madhara yanayo wakumba kwenye ngozi zao
hizo, kwa asilimia kubwa madhara yake yanatibika, ila pesa yake ya
matibabu ni ndefu, jambo ambalo ni cost kubwa sana kuanza kujitibu ni
bora kujiepusha kabisa na mambo hayo ya urembo wa muda.Hizi ni baadh tu
ya picha za wasanii wetu wa hapa Tzee ambao hutoweza amini jinsi
walivyobadilika, kabla na baada ya kupata umaarufu.
Wema Sepetu.
Ray-C.
Diva Loveness.
Vibe Magazine
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments