,

HEBU CHEKI HIZI PICHA, HEMED NA MZEE MAJUTO WAKIWA LOCATION

10:38 AM


Hemedy PHD na King Majuto wapo jijini Mwanza kushoot filamu yao mpya ya comedy iitwayo ‘Kimbulu’.
Hemedy akiwa na King Majuto

Hemedy ameiambia BK kuwa uamuzi wa kufanyia filamu hiyo jijini Mwanza ni kutaka kupata mazingira tofauti kwakuwa filamu nyingi za Tanzania hufanyika jijini Dar es Salaam.

Hemedy kama mwizi wa kuku

“Watu wengi wamekuwa wakisema kwamba wamechoka kila siku kuona majengo ya Dar es Salaam kwahiyo tumeamua kubadilika kuja huku halafu Mwanza yenyewe sio town ni kidogo nje ya mji. Nafikiri kutokana na mandhari ya Mwanza mawe mawe mtu atakuwa anajua kabisa kwamba project hii imefanyika ndani ya Rock City,” amesema.

Wanakijiji wakimfanyizia Hemedy

Akisimulia mkasa wa filamu hiyo, Hemedy amesema inawahusu vijana wawili wanatoka mjini wanakwenda kijijini kutafuta waigizaji wa filamu ili wawaunganishe na mastaa wakubwa wa filamu lakini wanapofika huko mambo hayaendi kama walivyokuwa wanatarajia na kujikuta wakifanya uzinzi tu.
“Kwahiyo inafika stage sasa kijiji kinajua tabia zetu mbaya tunawindwa sana na yule mzee mwenyewe ambaye ni babu yetu tulipofikia na yeye tabia yake hizohizo halafu anaentertain. Kwahiyo sisi tukipiga vitoto yenyewe anapiga wake za watu mpaka mwisho wa siku tunakuwa wezi kijijini kule,” ameongeza.
Hemedy akiwa na wakazi wa location ya jijini Mwanza wanakoshoot filamu mpya
Hemedy amesema lengo la filamu hiyo ni kuonesha hali halisi ilivyo kwenye tasnia ya filamu ambapo watu wengi hurubuniwa na matapeli.
“Kwahiyo ni kuwafungua macho wale wote wanaotumika kwa style hiyo na vilevile kuonesha wasanii kwamba kama tunaamua kusaidia tusaidie kweli na isiwe watu tunawafanyia michezo mibaya kama hiyo.”
Katika hatua nyingine, Hemedy amesema hataki kushirikishwa kwenye tuzo za Action n Cut.
“I really appreciate kwa wale waliohisi nafaa kuingia kwenye hizi tuzo hasa category ya best actor…ILA SIONI SABABU YA MASHABIKI ZANGU KUPOTEZA MUDA NA PESA ZA KUVOTE KWANGU!!!……IM NOT INTERESTED!!!…..TUZO YANGU IPO KWA MASHABIKI ALWAYZ.AND IM SO PROUD OF WHAT I DO!!!!…#PAPPINATION,” ameandika kwenye mtandao wa Instagram.

#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....