MSANII wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni
alijikuta akichezea kichapo kutoka kwa mpenzi wake anayejulikana kwa
jina la Amani baada ya kutaka kwenda klabu usiku bila kumtaarifu.
“Kwa kweli alipigwa sana na sasa amevimba uso,” alidai mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu lakini hawakuweza kuonana naye kwani aligoma akidai kwa hali aliyonayo hawezi kuonana na waandishi ila akasema:
“Ni kweli Amani kanipiga, kaniumiza ila siwezi kuliongelea sana suala hilo, haya ni mambo yetu binafsi.”
-GPL
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments