matukio,
mpya
MASIKINI MSANII HUYU!! ANAUMWA VIBAYA HALI YAKE SI NZURI...SOMA HAPA NA UMUOMBEE PIA
1:34 AMMASKINI! Hali ya kiafya ya msanii wa Komedi Bongo, Ismail Issa
Makombe ‘Mapembe’ inazidi kuwa mbaya kutokana na kuugua maradhi ya ini
kwa muda mrefu huku ikidaiwa kuwa wasanii wenzake wamemtelekeza.
Msanii huyo alifunguka kwamba alipimwa katika Hospitali ya Burhan, Dar na kuambiwa kuwa mwili wake umejaa sumu kwa asilimia 93 na ini limefeli huku akiwa ametokwa na vidonda usoni na tumbo lake kuvimba.
“Nimeamua kurudi nyumbani kwetu Mtwara ili angalau niombe msaada kwa ndugu na jamaa zangu niweze kuishi na kujaribu kupata matibabu zaidi.
“Hali yangu ni mbaya sana kwani mwanzo
nilikuwa nikisaidiwa na bosi wangu ambaye naye kwa sasa anaonekana
kuelemewa na majukumu yake, hivyo nawaomba sana wadau waweze kunisaidia
kwa sababu ninaumia sana.
“Imefikia hatua leo ninatambua kuwa wasanii wa filamu ni wanafiki,
maana tangu mwaka jana hadi leo ninaumwa lakini hakuna hata mmoja
aliyeweza kunisaidia zaidi ya Kitale ambaye alikuja kuniona,” alisema.Mapembe kabla hajaugua alikuwa akiigiza kwenye Kundi la Vituko Show kwa kuvaa uhusika wa aina mbalimbali lakini mara nyingi alikuwa akifiti sana alipokuwa akiigiza kama askari wa usalama barabarani ‘trafiki’.
Yeyote aliyeguswa na matatizo ya msanii huyu anaweza kumsaidia kwa kutumia fedha kwa Tigo Pesa kwa namba 0719 985659 au Airtel Money kwa namba 0784 328963.
GPL
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments