Wasanii wa muziki Shilole na Nuhu Mziwanda wameamua kuweka wazi
uhusiano wao wa kimapenzi na kudai kuwa wapo tayari kufunga ndoa.
Akizungumza na U heard ya XXL, Clouds FM leo,Shilole na Nuhu wamesema
wanapendana sana na wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya
miezi mitatu sasa.
“Tunajipanga mambo fulani yakae sawa pamoja na mke wangu kila kitu
kitakaa sawa,” alisema Nuhu. “Kweli tunakama miezi miwili ,mitatu
tunashukuru Mungu tunapendana kiukweli. Yeye ananipenda na mimi nampenda
pia, mimi nipo real kwake na yeye yupo real kwangu kila mtu yupo real
kwa mwezake. Nilikuwa na girlfriend kipindi hicho ila tumeachana,
tumegombana siunajua, na nimekaa muda mrefu bila kuwa na girlfriend,
yaani mambo yalifanya tukaonana tukapendana hivyo .First time nakumbuka
tulikutana studio,alikuja studio Kijitonyama ambapo mimi nilikuwa
nafanya kazi natengeneza beat zangu skeleton tukaongea mambo mengi ya
kimaisha hatukuwa in deep sana kihivyo, ila tulivyoendelea kujuana
tukaona kila mtu akamzoea mwenzie,mimi nikiwa mbali anakasirika na mimi
nikiwa mbali nay yeye anakasirika. Kwahiyo end of the day tukawa
tunapendana kweli yakawa mapenzi.”
Naye Shilole alidai kuwa ni kweli wanapenda na Nuhu.
“Sijamkana Nuhu,kwanini nimkane kwa sababu gani? Yeye ananipenda na
mimi nampenda,” alisema Shilole huku akisema yupo tayari kwa kufunga
ndoa na msanii huyo.
CREDIT : BONGO5
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments