Mapacha
wawili walioungana kiwiliwili, Maria Mwakikuti (kushoto) na Consolata
Mwakikuti (kulia) wakila chakula katika hafla ya kuwapongeza kwa kufaulu
mtihani wa darasa la saba mwaka 2010 katika hospitali ya misheni Ikonda Makete
Aliyekuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Getrude Mpaka akiwapa zawadi ya vitabu
mapacha wawili walioungana kiwiliwili, Maria Mwakikuti (kushoto) na
Consolata Mwakikuti (kulia) baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba
mwaka 2010
WENGI
wamesikia historia ya wale mapacha walioungana kiwiliwili; baada ya
kimya chao cha muda mrefu wengi watapenda kujua wako wapi na wanafanya
nini?
Wanafunzi hao Maria Mwakikuti na Consolata Mwakikuti
wanasoma shule ya sekondari ya Nyota ya Asubuhi iliyopo Kidabaga,
wilayani Kilolo mkoani Iringa.
Uongozi wa shule umeweka masharti
magumu kidogo ili kukutana nao, lakini mtandao huu unaendelea
kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo ili watanzania waweze kujua
maendeleo yao.
Kwa wasiofahamu mapacha hao, ni wenyeji wa wilaya
ya Makete mkoani Njombe; wilayani humo wanaishi katika kijiji cha
Ikonda, hapo ndipo walipozaliwa na kumalizia elimu yao ya msingi.
Walipokuwa
wakimaliza elimu ya msingi, walikuwa na umri wa miaka 13 na katika
ndoto zao kwa pamoja walisema wanataka kuwa wataalamu wa kompyuta.
Miaka
mitatu sasa imepita toka wawakilishi wa mtandao huu wakutane nao katika
hafla ya kuwapongeza baada ya kufaulu vizuri mitihani yao ya darasa la
saba.
Wapo kidato cha nne katika shule hiyo ya Nyota ya Asubuhi;
walijiunga na shule hiyo baada ya walezi wao kukataa wasijiunge na shule
ya sekondari ya Jangwani walikokuwa wamepangiwa baada ya matokeo yao
kutoka
Hivi sasa wana miaka 17. wanaukaribia utu uzima, kwa
vyovyote watakuwa na mengi ya kuzungumza kuhusu maisha yao ya sasa,
elimu yao, changamoto wanazopata na matarajio yao ya baadayE
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments