matukio,
mpya
MSANII WA TUSKER PROJECT FAME AAMUA KUWA MUASI, TAZAMA NA SOMA ALICHOANDIKA HAPA
2:07 AM
Msanii wa Project fame alieingia kwenye vita ya nchi, anasema Rais akiuwawa amani ndio itakuja.
Unaweza kujaribu kutengeneza picha, pale ambapo msanii anaamua kushika bunduki na kuingia kwenye vita ya nchi yake kisa hajapendezwa na upande mmoja kati ya mbili zinazopingana.
Imeripotiwa kwamba huenda aliewahi kuwa mshiriki wa shindano la Tusker Project fame Kuonck ‘K-Denk’ Deng na kuiwakilisha nchi yake ya Sudan ya Kusini, ameamua kushika silaha na kuingia vitani.
Kwenye page yake ya facebook, K Denk amepost status kadhaa zenye utata ambazo mapokezi yake hayajawa mazuri… na hii imeonekana toka vita ianze December 2013 nyumbani kwao Sudan.
Updates zinaonyesha msanii huyu alieamua kuingia vitani, amehama kutoka Juba hadi sehemu ya kaskazini ambayo inashikiliwa na Waasi.
K Denk ameonekana kuwa upande wa Waasi wanaopigana na Serikali huku akisisitiza kwamba amani itapatikana baada ya Rais Salva Kiir kuuwawa.
Baadhi ya mashabiki zake ambao ni sehemu ya waliopoteza ndugu zao kwenye vita hii hawajasita kumuandikia ya moyoni.
0 comments