AINA
kadhaa za kuku weusi hupatikana barani Asia, lakini kuku au ndege
aina ya Silkie wa huko China, ndiyo maarufu zaidi. Ndege hao, kama
majina yao yalivyo, huwa wana manyoya yanayofanana na hariri.
Hata hivyo, chini ya uzuri wote huo, ndege hao wana ngozi
nyeusi tii! Ndege hao huuzwa katika nchi za magharibi kama mapambo,
ambapo nchini China ni kitoweo cha hali ya juu kwani nyama yake
hupendwa sana. Pia ndege hao huchukuliwa kama ‘mama wema’ kwani
wanaweza kuatamia mayai ya ndege wengine bila kinyongo.
Wachina huwaelezea ndege hao kama “kuku wenye mifupa
myeusi” au “wu gu ji” na wamekuwa wakiwala kwa kuamini nyama yao ina
tiba tangu karne ya saba au ya nane ambapo wanawake huila kwa ajili ya
kuimarisha afya zao baada ya kujifungua. Pia nyama hiyo inaaminika
kuimarisha mapafu, tumbo na damu ikiliwa. Wachina huitumia nyama ya
ndege hao kwa kutengeneza supu yake na kuichanganya na viungo na matunda
mbalimbali kwa ajili ya tiba.
Utafiti uliofanywa na kuchapishwa mwaka 2011 ulionyesha
kwamba hali hiyo ya kipekee ya ndege hao aina ya Silkie ambayo
inajulikana kama ‘fibromelanosis’ inatokana na mabadiliko katika jeni.
Mabadiliko hayo kisayansi huenda sambamba na kuongezeka kwa
chembechembe za rangi ambazo huzifanya sehemu za ndani (mwilini) na
mifupa kuwa nyeusi.
Ndege hao pia wana chembechembe za aina ya ‘carnosine’
ambazo huongeza nguvu mwilini. Watu wenye kutaka kuongeza ukubwa wa
misuli huwatumia kwa wingi kwa nia hiyo na kama chakula chenye kuleta
nguvu. Pia hutumika katika kupambana na ugonjwa wa akili wa watoto
(autism), kisukari na kupambana na matatizo yanayotokana na uzee.
Kwa jumla ndege hao hutumiwa kama tiba ya maumivu ya viungo na kuzuia ugonjwa wa akili ujulikanao kama Alzheimer.
Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi kuhusu kuku nchini
Uingereza, mayai ya kuku weusi ni bora kwa afya hasa yakitumika katika
kupika keki. Yakilinganishwa na mayai mengine, mayai ya kuku weusi yana
kiwango kidogo cha tindikali katika mafuta yake. Kwa waliowahi kuila
nyama yake, wanasema ina ladha kama ya kuku wa kawaida, lakini baadhi
hudai ni tamu zaidi. Je, ungependa kula nyama ya Silkie ili ufahamu
utamu #SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments