matukio,
mpya
MKE AFUMANIWA, AAGA ANAENDA KWA BIBI KUMBE KAENDA KUJIUZA...CHEKI PICHA NZIMA HAPA
8:08 AM
OPARESHENI
Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers si mchezo! Safari hii imenasa
tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose kuuza mwili.
Tukio
hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya mji
kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na
polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu ya
ngono.
Kwa
mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa
anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni mgonjwa.
Tofauti
na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo
hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha
ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari
15, mwaka huu.
Mshangao: Mchumba wa mtu akishangaa baada ya kubambwa na OFM.
Jumatano
iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alieleza kuwa
kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika viunga vya
Kaumba.
Dada
huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha
harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini
alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.
Twendeni: Mchumba wa mtu akiongoza wenzake wanaoshuka kutoka kwenye difenda kuelekea kituoni.
“Niamini
mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za advance ya
ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake inatarajiwa
kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.
Chini ya ulinzi: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa chini ya ulinzi kituoni.
OFM
ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao walimtia
mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa wanaume huku
mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia
chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
Hata
hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye na
wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha
polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake.
SOURCE: GPL
#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#
0 comments