,

PREZO AMUITA DIAMOND 'MWAJUMA', SOMA ALICHOPOST HAPA

10:56 AM


Wakati huu unaweza kuwa wakati wa kucheka kiaina kwa Huddah Monroe ambaye kwa kipindi kirefu alinyimwa raha na tambo za mrembo wa kitanzania aishie Marekani, Starlisha Tillya aka Chagga Barbie au The First Lady ambaye alikuwa analimiliki penzi la mfalme wa bling bling Jackson Makini aka Prezzo.
Hali imebadilika sasa na inaonesha dhahiri Starlisha na Prezzo wamepigana chini, na hasira zimemsababisha mrembo huyo amechukua uamuzi wa kupost kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya message za Prezzo alizochart naye zinazomponda mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
“Kufanya nyimbo na Davido kalipa $3000 wala davido hajam acknowledge kabisa.” Inasomeka message ya Prezzo, “Kiingereza Shida huh” inasomeka message nyingine, huku mrembo huyo akionesha kushangaa, “Mbona nasikia Davido kamualika!.”
Starlisha amemponda Prezzo na kumwagia maatusi katika post kadhaa na kudai kuwa mkali huyo wa ‘Lighter’ humuita Diamond Mwajuma.
 chagga-2
“Unatengeneza ma video yasiyo na kiwango Kutwa kumponda Diamond Mara ngapi nimemtetea huyu kinara wa East Africa usiyemkubali wewe unamuita mwenzio sijui Mwajuma wewe na yeye Nani Mwajuma kaa sio wewe. Natafuta namba ya kuweka ur voice notes watu wakusikilize kibuyu wewe.” Yanasomeka maandishi haya kwenye post nyingine iliyomalizika kwa matusi ya makali ya nguoni.
Chagga Barbie amedai kuwa Prezzo amekuwa akimbembeleza amuwish birthday kwa kumpost kwenye mitandao ili aonekane, lakini pia kumuomba ticket na kuomba mrembo huyo amnunulie Sneakers.
Mwaka jana Prezzo aliingia katika beef na Diamond Platinumz kutokana na maandishi ya gazeti moja la Kibongo, lakini Prezzo alimuomba msamaha Diamond aliyetaka aombwe msamaha huo kupitia mitandao ya kijamii kama alivyomponda kupitia mitandao hiyo. Kitu ambacho Prezzo alikiita ‘Utoto’.
Hata hivyo beef hilo liliyeyuka.
credit : times fm 


#SHARE THIS NEWS AND WIN!!!#

You Might Also Like

0 comments

JIUNGE UPATE HABARI

Jisajili Sasa upate E-mail ya Kila Tunachochapisha....